MAN UNITED YAIFUNGA FULHAM 3-2,TAZAMA MATUKIO YOTE HAPA Robin van Persie amefunga bao lake la kwanza Manchester United na kukiwezesha kikosi cha Sir Alex Ferguson kuibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya Fulham, Uwanja wa Old Trafford. Van Persie, ambaye alitokea benchi kuingia uwanjani Jumatatu United ikifungwa na Everton baada ya kukamilisha uhamisho wa pauni Milioni 24 kutoka Arsenal, alipewa nafasi leo, wakati Wayne Rooney akianzia benchi. Robin van Persie akifunga bao lake la kwanza Manchester United Van Persie akipongezwa ma wenzake baada ya kuifungia bao Manchester United Robin van Persie akifurahia bao lake la kwanza akiwa na jezi ya Manchester United Shinji Kagawa akiifungia United Shinji Kagawa akishangilia. Rafael (Namba 2) aliifungia Manchester United Rafael akishangilia bao lake Kipa wa Fulham, Mark Schwarzer
Posts
Showing posts from August 25, 2012
- Get link
- X
- Other Apps
Man Utd 3 Van Persie 10′ Kagawa 35′ Rafael 41′ Fulham 2 Duff 3′ Vidic 64′ (og) Robin Vav persie score 25 August 2012 Last updated at 16:52 GMT By Alistair Magowan BBC Sport at Old Trafford Robin van Persie crowned his full debut for Manchester United with a stunning first goal for his new club in a nervy win against Fulham. The Dutchman's strike came after Damien Duff had given the visitors the lead, and it came in a scintillating first half as Shinji Kagawa ...
- Get link
- X
- Other Apps
Van Persie set to start to day. Saturday 25th August 2012 12.45pm: Swansea City v West Ham United #SWAWHU 3.00pm: Aston Villa v Everton #AVLEVE 3.00pm: Manchester United v Fulham #MUNFUL Full match preview>>> 3.00pm: Norwich City v Queens Park Rangers #NORQPR 3.00pm: Southampton v Wigan Athletic #SOUWIG 3.00pm: Sunderland v Reading #SUNRDG 3.00pm: Tottenham Hotspur v West Bromwich Albion #TOTWBA 5.30pm: Chelsea v Newcastle United #CHENEW Sunday, August 26th 1.30pm: Stoke City v Arsenal #STKARS 4.00pm: Liverpool v Manchester City #LIVMCI .
- Get link
- X
- Other Apps
Nyota 10 wafupi zaidi Ligi Kuu England. Santiago Carzola LONDON, England LIGI Kuu England haikosi vituko. Licha ya kuwa yenye ushindani mkubwa dimbani, pia ligi hiyo inajivunia kuwa na wachezaji warefu na wafupi. Miongoni mwa wachezaji wapya wa ligi hiyo, Santi Cazorla wa Arsenal ni mmoja wa wageni ambaye ameingia katika kumi bora. Yeye ni mmoja wa wachezaji kumi wafupi zaidi kwa kimo wenye urefu wa futi 5 inchi 5, 6 na 7. Baada ya kusajiliwa kwa pauni 15 kutoka Malaga, kiungo huyo aling'ara katika mchezo wa ufunguzi wa msimu dhidi ya Sunderland, Jumamosi. Umahiri wake wa kuchezea mpira, kutoa pasi murua umemfanya Cazorla ambaye ameichezea Hispania mechi za kimataifa 49 awe na kitu zaidi cha kujivunia. Lakini, si yeye pekee ambaye ni mfupi zaidi katika Ligi Kuu England, wapo wengine tisa. ...
- Get link
- X
- Other Apps
Bao la 'offside' la Torres laibeba Chelsea LONDON, England MSHAMBULIAJI Fernando Torres alifunga bao la utata na kuisaidia Chelsea kupata ushindi mnono wa mabao 4-2 dhidi ya Reading kwenye Uwanja wa Stamford Bridge. Utata wa bao Torres ulikuja baadaye picha ya televisheni ilionyesha mshambuliaji huyo wa Hispania alikuwa ameotea wakati akiunganisha krosi ya Ashley Cole. Msimu uliopita Torres hakufunga bao lolote hadi mwezi Septemba 18na kufanikiwa kumaliza akiwa amefunga mabao sita tu.. Ni wazi alikuwa ameotea nimeuzunika sana, alisema kocha wa Reading, Brian McDermott, ambaye alipiga bao hilo kwa mwamuzi msaidizi. Ni aibu kubwa kwa mwamuzi kuruhusu bao kama ilo. Reading waliamka kusaka bao la kusawazisha, lakini Eden Hazard alifanikiwa kuzuia mpira wa adhabu na kuanzisha shambulizi la ...
- Get link
- X
- Other Apps
Timu za Tanzania zateswa Uganda KAMPALA, Uganda TIMU za Tanzania zimeanza vibaya mashindano ya kikapu ya Kanda ya tano yanayofanyika Kampala, Uganda. Timu za Tanzania zinazoshiriki mashindano hayo ni ABC, Jeshi Stars, Don Bosco na Savio. ABC wenyewe walianza kwa kufungwa 73-85 na D-Mark Power, wakati Eagle Wings iliichapa 92-36 Donbosco, huku Jeshi Stars ikichapwa 47-84 na Berco Stars. Pia katika mechi zilizofuata timu ya Urunani iliichapa Savio 58-51, wakati KCB iliichapa ABC 95-59 na KPA iliishinda Jeshi Stars 91-38. Juzi timu ya D-Mark Power kutoka Sudan ya Kusini iliichapa ABC 85-73 na kuingia hatua ya nusu fainali. Wakati huohuo Mwenyekiti wa Baraza la Michezo wa Uganda (NCS), Anthony Katamba amejiuzulu wadhifa wake kwa sababu ya mgogoro wa kuutumia uwanja wa ndani wa Lugogo unaoandaa mash...
- Get link
- X
- Other Apps
Pacha wa Mbuyu kujiunga Yanga Yanga wakishangilia bao wakiongozwa na Hamis Kiiza na Mbuyu Twite DORIS MALIYAGA, KIGALI MNYARWANDA Mbuyu Twite amefuta ukimya na kuzungumzia ujio wa pacha wake katika timu ya Yanga. Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwanaspoti, Mbuyu alisema Yanga imemwahidi kumsajili pacha wake, Kabange Twite wakati wa Dirisha Dogo la usajili Novemba mwaka huu. "Kweli Yanga waliniambia watamsajili, Kabange na nitacheza naye hapo baadaye. "Lakini kabla ya hapo atakuja Dar es Salaam nitakuwa naye mara tu atakapotoka Congo," alieleza Mbuyu na kubainisha kuwa kwa sasa Kabange anafanya mazungumzo na Lupopo ya Congo baada ya kumalizana na APR ya Rwanda. Mbuyu alisema licha ya kumkosa pacha wake, ambaye kwa kawaida lazima wacheza timu moja, alisema ...
- Get link
- X
- Other Apps
Kitaeleweka: Liverpool, Man City zatunishiana misuli Kocha wa Man City Roberto Mancini ONDON, ENGLAND LIGI Kuu England imeanza tangu wiki iliyopita, lakini utamu halisi utaanza kesho Jumapili wakati Liverpool na Manchester City zitakapokwaana katika Uwanja wa Anfield. Kila kikosi kitaingia uwanjani kusaka ushindi, Manchester City inataka kuendeleza ubabe baada ya kuinyoa Southampton mabao 3-2 wikiendi iliyopita ikiwa ni ushindi wa tano katika mechi tano za karibuni. Kwa upande wake, Liverpool haiwezi kukubali kuwa wateja kwa mara nyingine kufuatia kufungwa mabao 3-0 na West Brom wiki iliyopita. Manchester City inakwenda katika mechi hiyo ikiwa na historia nzuri katika siku za karibuni, lakini timu hizo zilipokutana katika mechi tano za nyuma, Liverpool ilipata ushindi mara mbili, Manch...
- Get link
- X
- Other Apps
KASEJA ATOKEZEA IKULU KIGALI, RWANDA KATIKA mazingira ya kutatanisha kipa wa Simba, Juma Kaseja aliitwa kuingia katika msafara wa Yanga uliokwenda kwa Rais wa Rwanda, Paul Kagame juzi Alhamisi usiku kwenye Ikulu ya nchi iliyoko mjini Kigali. Mmoja wa walinzi wa Kagame ndiye aliyeboronga baada ya kutaja jina la kipa huyo kama miongoni mwa watu waliokuwamo kwenye msafara huo ulioongozwa na Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Fatuma Karume. Jina la Kaseja lilifumuka wakati mlinzi huyo wakati akisoma majina ya msafara wa Yanga waliokuwa wamealikwa na Rais Kagame. Yanga walikwenda kumwona Kagame, ambaye alitaka kuwapongeza baada ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Kagame. Sinema nzima ilianza hivi: Yanga walipofika Ikulu kulitakiwa kuwasilisha majina kamili ya wahusika wote watakaoingia ndani ikiwa ni hatua ya kudhibiti usalama kama ilivyo kawaida watu wanapotembelea sehemu nyeti kama Ikulu. Mlinzi huyo alikuwa na orodha ya majina hayo na alikuwa akiita watu kwa sauti na kil...