Hamilton ashinda mbio za Hungary. Dereva wa Timu ya magari ya McLaren, Lewis Hamilton alijikuta katika sayari yake mwenyewe kwa kuongoza mbio za magari ya Hungary hadi mwisho. Dereva huyo Muingereza aliweza hata kuweka kasi ya kupindukia kwenye mizunguuko miwili, iliyomuwekea mda wa kuweka pengo la sekunde 0.413. Dereva wa magari ya Lotus Romain Grosjean alifuata wa pili mbele ya Sebastian Vettel wa timu ya magari ya Red Bull. Muingereza Jenson Button wa magari ya McLaren alimaliza wa nne, Kimi Raikkonen wa 5, Fernando Alonso akamaliza wa 6 huku Mark Webber akimaliza wa 11. Nafasi ya 10 ilifunikwa na Felipe Massa wa magari ya Ferrari aliyefuatiwa na Pastor Maldonado wa timu ya magari ya Williams akafuata Bruno Senna, na Nico Hulkenberg wa kikosi cha Force India. Hamilton alisema baada ya mbio kuwa: "ni afuweni kubwa kuona matunda ya marekebisho tuliyoyafanya na nimefurahishwa kuona kwamba nimelitumia gari ninavyotaka. Uwezxo wa magari ya Ferrari leo umedhihiris...
Posts
Showing posts from July 29, 2012
- Get link
- X
- Other Apps
RAIS KIKWETE AFUNGUA KONGAMANO LA TATU LA JUKWAA LA UHUSIANO WA CHINA NA AFRIKA KATIKA KUPUNGUZA UMASKINI. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Kongamano la tatu la Jukwaa la Uhusiano wa China na Bara la Afrika katika kuondoa umaskini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam jana Julai 28, 2012. Wa tatu toka kushoto ni Waziri wa China anayeshughulikia Umaskini Mhe Fan Xiaojian, wa pili kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya rais Mhe Steven Wassira, wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Fedha na Maendeleo ya Uchumi wa Sierra Leone Mhe Momodu Kargbo, kushoto ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Dkt Philip Mpango na kulia kabisa ni Balozi wa China hapa nchini Mhe L.V. Youqing. Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha na ujumbe toka China unaohudhuria Kongamano la tatu la Jukwaa la Uhusiano wa China na Bara la Afrika katika kuondoa umaskini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam jana Julai 28, 2012. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Wazi...