BI HARUSI HAFA MAJI BWANA HARUSI APONA. HUKU majonzi yakiwa bado yametawala miongoni mwa Watanzania kufuatia vifo vya watu waliokuwa ndani ya meli ya MV Skagit ambayo ilipinduka na kuzama Julai 18, 2012 karibu na Kisiwa cha Chumbe, Zanzibar mambo mengi yameibuka. Nje ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik siku ya Jumatano (juzi) ambako serikali ilikuwa ikitoa ripoti ya maendeleo ya uokoaji, baadhi ya watu walikuwa katika hali ya majonzi kufuatia ndugu zao kutojulikanna walipo. Hamis, aliyedai ni mfanyakazi wa Kampuni ya Azam ya tajiri Said Salim Bakheressa alisema mdogo wake, Khalfan na mchumba wake, Zaina Ally walikuwa ndani ya meli hiyo kwenda Zanzibar kufunga ndoa Alhamisi (juzi) kama maandalizi ya kuukaribisha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, lakini mpaka siku hiyo mdogo wake aliokolewa, ila Zaina hajulikani alipo. Hamis alisema: “Naamini shemeji yangu amefariki dunia, kwani katika watu wote waliokolewa hayupo, maskini mdogo wangu (Khal...