Posts

Showing posts from August 23, 2012
Tuseme yetu, waseme yao kwa Katiba bora. TUME ya Mabadiliko ya Katiba imetangaza kuanza kwa awamu ya pili ya mchakato wa kukusanya maoni ya Watanzania, kuhusu kuandikwa kwa Katiba mpya ya nchi. Uamuzi wa tume kutangaza awamu hiyo ya pili unatokana na kukamilika kwa awamu ya kwanza. Katika awamu ya kwanza, tume imezuru mikoa minane Tanzania Bara pamoja na Zanzibar, ambako imekutana na wananchi na kuwasikiliza. Tathmini inaonesha kwamba kuna kasoro ndogo zilizojitokeza katika awamu hiyo ya kwanza, ingawa pia kuna mafanikio kwa kiasi kikubwa. Kati ya kasoro hizo ni pamoja na zilizopata kuzungumzwa na Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji (mstaafu) Joseph Warioba, hususan madai ya kuwapo kwa baadhi ya wanasiasa, ama moja kwa moja au kupitia vyama vyao, wanaopandikiza mawazo yao yanayo...
Image
Mbunge ahusishwa na ‘wauzaji’ bangi. MBUNGE wa Viti Maalumu kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kutokea mkoani Tabora, Munde Tambwe Abdallah, anahusishwa na wanawake waliokamatwa wakisafirisha bangi kwenda nje ya nchi, Raia Mwema limefahamishwa. Raia Mwema limejulishwa kwamba mmoja wa watuhumiwa waliokamatwa na bangi na kufikishwa mahakamani, Hadija Magesa ni ndugu wa mbunge huyo na jina lake halisi ni Hadija Tambwe Abdallah, na kwamba walikuwa pamoja muda mchache kabla ya wote kuanza safari kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Taarifa zilizopatikana zinaonyesha kwamba Munde aliondoka nchini kwa ndege ya Shirika la Ndege la Emirates namba EK 726, Julai 28, 2012 kwenda Italia, saa chache kabla ya Hadija na mwenzake, Sasha Mnyeke, kukamat...
Image
Wachezaji wavuta bangi kukiona. •  TFF yatunga sheria kuwabana SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limesema litaanza kufanyia kazi kwa vitendo tatizo la utumiaji wa dawa za kulevya hususan bangi unaodaiwa kufanywa na baadhi ya wachezaji hapa nchini. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Rais wa TFF, Leodegar Tenga, alisema miongoni mwa changamoto kubwa zinazowakabili ni kile kinachodaiwa kuwa baadhi ya wachezaji wanatumia bangi, ingawa bado hawajapata ushahidi. “Tunasikia, lakini hatuna ushahidi, kwamba vijana wetu wanatafuna bangi, ila viongozi wengi wamekuwa wakilisemea pembeni, sisi kama wazazi jukumu letu ni kuwaelimisha juu ya athari zake, maana wao wanaotumia wanaweza kuona inawaongezea hamasa, lakini hawajui madhara yake,” alisema Tenga. Alisema wameagiza suala hilo lianze kufanyiwa kazi katika timu ya taifa, Taifa Stars na Ligi Kuu Bara, ambako viongozi wanapaswa kukaa chini na vijana wao kuwapa elimu nasaha, kabla ya kuanza kuchuk...
Vodacom yatengeneza ajira zaidi kwa Watanzania. KAMPUNI ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, imetangaza kujivunia wingi wa ajira ambazo imetengeneza kwa Watanzania tangu kuanzishwa kwake. Kampuni hiyo imeajiri asilimia kubwa ya Watanzania katika ajira za moja kwa moja na zile zisizo za moja kwa moja. Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Rene Meza, alitaja maeneo mbalimbali ambayo kampuni hiyo imetoa ajira kwa wingi kuwa ni huduma ya M–pesa ambayo imetengeneza ajira zaidi ya 25,000 kwa watu wa makundi mbalimbali. “Kama kampuni tuna ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja, kupitia huduma yetu ya M-pesa, sasa tumetengeneza ajira zaidi ya 25,000 hapa nchini; mijini na vijijini. “Hii ni hatua kubwa sana katika sekta ya ajira. Kwa kuwa huduma hii imeshika hatamu katika huduma za kifedha bado watu wengi zaidi wanaendelea kujiunga na uwakala. Kwa mwezi sasa tunapata maombi ya uwakala zaidi ya 2,000 hivyo tunatarajia ajira hizi kuongezeka kwa kasi,” a...
Walimu wampa DC siku saba. CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT), kimempa siku saba Mkuu wa Wilaya (DC) ya Mbeya, Dk. Norman Sigalla kwa madai kuwa aliwakashifu walimu na chama hicho kwa ujumla wakati wa semina za sensa ya watu na makazi hivi karibuni. Taarifa ya CWT kupitia barua yao iliyosambazwa kwenye vyombo vya habari na katibu wake, Kasuku Bilago, ilisema kuwa wamepokea malalamiko kutoka kwa walimu juu ya DC huyo jinsi alivyowakashifu wakati wa semina. Ilisema kuwa kwa nyakati tofauti, mkuu huyo alipita kwenye vituo vya semina hizo ambazo wengi walikuwa walimu na kutoa kashfa dhidi yao na chama chao. Barua hiyo ya Agosti 21 mwaka huu, kwenda kwa mkuu wa wilaya imeeleza kuwa baadhi ya kashfa alizotoa ni kwamba walimu ni kada ya waliofeli mitihani na hivyo serikali inawashangaa kudai waongezewe mishahara. “Ulieleza kuwa walimu wamejaa madudu kichwani, ni manjuka yaani watu mbumbumbu wasiojua kitu chochote, kuwa Gratian Mukoba (Rais wa CWT) anamiliki...
Image
Tanzania imejaaliwa kuwa na aina nyingi sana za wanyama katika mbuga zetu. Na wao kama viumbe hai kuna wakati wanapata magonjwa yanayotishia uhai wao. Ungekuwa wewe ni daktari wa wanyama ungepata ujasiri wa kutibu wanyama wakali kama Simba, Chui, Mamba au Nyoka
Mrwanda kutimkia Ufaransa . BAADA ya kufunga ndoa Danny Mrwanda ameweka bayana kuwa anadhamiria kutimkia Ufaransa, Mwanaspoti lina taarifa kamili. Nyota huyo ana malengo ya kwenda huko na ikishindikana atarudi Vietnam alikokuwa akicheza soka lake awali. "Natarajia kuondoka kwenda Ufaransa kwa mujibu wa wakala wangu, lakini ikishindikana nitarudi Vietnam nilikokuwa nacheza awali. "Nitaondoka baada ya kufunga ndoa Septemba 7 lakini nasubiri barua ya kuachwa kutoka Simba,"alisema. Akizungumzia kuachwa kwake, Mrwanda alisema ni jambo la kawaida katika maisha ya soka. Mrwanda hajajumuishwa katika kikosi cha Simba kitakachocheza msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara licha ya kufikia nayo makubaliano na kucheza mechi za Kombe la Urafiki na Kagame ingawa alishindwa kuonyesha kiwango. Kocha mpya Azam akuna kichwa KOCHA Mkuu wa Azam FC, Mserbia Boris Bunjak amekiri yupo katika wakati mgumu kipindi hiki kukirudishia makali kikosi cha timu hiyo yenye maskani yake Cham...
Image
Chicharito ni Man United tu.   Mexico City, Mexico BABA ya mshambuliaji wa Manchester United, Javier Hernandez ameibuka na kupinga madai ya nyota huyo kutaka kuondoka Old Trafford. Vyote vinavyosema ni tetesi tu, Chicharito anamkataba na Manchester United na anataka kubaki hapo, Javier Hernandez Sr. alilimbia gazeti la Record la Mexico. Tangu kusajiliwa kwa Robin van Persie, kumekuwa na tetesi za kumhusisha Chicharito na kutimkia Arsenal, Juventus au Chelsea, wanaoripotiwa kuandaa dau kubwa kwa ajili ya mshambuliaji huyo. Katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu uliocheza Jumatatu dhidi ya Everton, Chicharito alikuwa mshambuliaji pekee wa United ambaye hakukaa kwenye benchi la timu hiyo. Katika miaka yake miwili aliyokuwa na klabu hiyo, Chicharito amefunga mabao 32 katika michezo 81 aliyocheza kwenye mashindano yote. Wakati huo huo; Siku za Nani ndani ya kikosi cha Manchester United zimeanza kuhesabika baada ya kuonyesha kiwango cha chini katika mchezo wa Jumatatu ...
Image
Hatimaye makarani wa Sensa walipwa .  Waandishi Wetu SIKU moja baada ya makarani wa Sensa ya Watu na Makazi kugoma kula kiapo cha utii na kutunza siri, Serikali imewalipa posho zao ili kuendelea na kazi hiyo.  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana alisema makarani ambao hawakuwa wamelipwa posho zao, Serikali imeshawalipa na hakuna karani anayedai posho katika wilaya hiyo. Rugimbana aliyasema hayo jana Dar es Salaam baada ya makarani zaidi ya 800 juzi kutishia kugoma kula                                                                                  kiapo cha ...
Image
Sumaye ajitosa Nec CCM. KUPAMBANA NA DK NAGU HANANG’, KIMBISA, GUNINITA, MABINA, KIGWANGALLA NAO WACHUKUA FOMU Waandishi Wetu BAADA ya kuwa kimya kwa muda mrefu, Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye amejitokeza tena katika ulingo wa siasa baada ya jana kuchukua fomu za kuwania Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Wilaya ya Hanang’ Mkoa wa Manyara akichuana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji), Dk Mary Nagu.Mara ya mwisho kuingia katika ulingo wa kuomba kura kwa Sumaye ambaye alikuwa Waziri Mkuu kwa kipindi chote cha miaka 10 ya utawala wa Awamu ya Tatu chini ya Benjamin Mkapa, ni mwaka 2005 wakati alipoomba kuchaguliwa na CCM kuwa mgombea urais na kushindwa. Katika uchaguzi wa Hanang’, Sumaye anachuana na Nagu ambaye alimwachia kiti cha ubunge katika Jimbo la Hanang' huku duru za siasa kutoka ndani ya chama hicho mkoani Manyara zikieleza kuwa hiyo inatokana na uhusiano wa kisiasa wa vigogo hao sasa kutokuwa mzuri. Uchukuaji huo w...