Uchaguzi Igunga na Pepo za Mabadiliko Tanzania Kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu Tanzania wa Oktoba 2010, tumeshuhudia pepo kubwa sana zikivuma kwa kasi kutoka pande zote za nchi yetu. Ni pepo za mabadiliko. Wananchi wanataka madadiliko ya kweli. Watawala walioko kwenye ngazi kubwa za nchi hii ama wamezisikia au kuziona hizo pepo lakini bado hawajaonesha jitihada za kuzizuia. Ni mwanzo wa miti mikubwa yenye nguvu kubwa (Key Politicians) kuangushwa chini na pepo hizo. Ni wakati ambapo watawala hawataamini kilichofanyika. Mabadiliko haya yamenikumbusha Hotuba makini na ya kihistoria ya Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Mr Hrold Macmillan alipotembelea Afrika na tarehe 3 Februari 1960 na akahutubia maelfu ya watu huko Afrika ya Kusini, na kusema: "The wind of change is blowing through this continent (Africa), and whether we like it or not, this growth of national consciousness is a political fact. We must all accept it as a fact, and our nationa...
Posts
Showing posts from August 22, 2012
- Get link
- X
- Other Apps
PICHA YA MHESHIMIWA RAIS AKIWA SHAMBANI KWAKE MSOGA. Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa na mjukuu wao Aziza Ridhiwani (3) katika ghala ya mahindi yaliyovunwa kwenye shamba lao kijijini Msoga, nje kidogo ya mji mdogo wa Chalinze, Mkoa wa Pwani. Rais Kikwete ni mkulima na mfugaji kijijini hapo na ameonesha kufurahishwa sana na mavuno makubwa ya mahindi shambani kwake. Hii katika kutekeleza kwa vitendo sera ya Serikali ya kuendeleza kwa ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya sekta ya kilimo katika Tanzania.(PICHA NA IKULU).