Venus hana lake Wimbledon Bingwa mara tano katika mashindano ya tennis ya Wimbledon, Mmarekani Venus Williams, amesema hana nia ya kustaafu, baada ya kuondolewa katika siku ya kwanza ya mashindano ya mwaka 2012 ya Wimbledon, katika raundi ya kwanza, aliposhindwa na mchezaji kutoka Urusi, Elena Vesnina. Venus, mwenye umri wa miaka 32, na anayeugua ugonjwa unaofahamika kama Sjogren's Syndrome , alishindwa 6-1 6-3 siku ya Jumatatu. Mpinzani wake Vesnina amepangwa katika nafasi ya 79 katika orodha ya wachezaji bora zaidi wa tennis wa kike ulimwenguni. "Haiwezekani nipumzike tu na kukata tamaa," alielezea Williams. "Sina muda wa kujisikitikia. Hilo sio jambo zuri. Nitautumia muda wangu katika mawazo yanayonipa nguvu. Ninaupenda mchezo huu." Mara ya kwanza Williams kushindwa katika rau...
Posts
Showing posts from June 26, 2012