Posts

Showing posts from August 13, 2012
Image
HUYU NDO SHUJAAAA WA UKWELI NA SIO HAO. Huyu ndiye John Stephen Akhwari shujaa wa Tanzania ambaye katika Olympic mwaka 1968 aligoma kuacha kukimbia baada ya mguu wake kuteguka na kujeruhiwa vibaya hadi alipomaliza na kutoa kauli ya "Nchi yangu haikunituma maili 10,000 kuja kuanza mbio bali kuja kumaliza mbio". Mwaka 1983 alipewa tuzo ya kipekee ya heshima kwa ushujaa wake na amekuwa akikaribishwa katika kila mashindano ya Olimpiki kama balozi wa heshima. Anakufundisha nini katika maisha yako ya kawaida.
Image
NGORO NGORO HEROES  YATOKA   MIKONO   NYUMA  KWA NIGERIA . Timu ya ngoro ngoro  imetolewa kwa idadi ya magoli 4-1,ambayo mechi ya kwanza ilitoka kwa kufungwa  2-1 na pili kwa kupigwa 2-0 hiyo na kufikisha idadi ya magoli 4-1 dhidi ya nigeria. Huwa najiuliza lini na sisi tutakuwa kama wenzetu ambao wanafanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa na kitaifa pia sasa sisi hatuna kitaifa wala kimataifa kote tunafanya vibaya  nachukia sana halafu viongozi hy hali wanaiyona ila wanaifanyia makusudi . Tujilekebishe na Tujiandae kutengeneza timu ya ukweli na sio ujanja ujanja wa mjini. kikosi cha ngoro ngoro heroes kikiwa kwenye picha ya pamoja
Image
TWITE AKABIDHIWA JEZI YANGA. Mbuyi Twite beki mpya wa Klabu ya Yanga akikabidhiwa uzi wake mpya na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Yanga Abdallah Bin Kleb. Mchezaji huyu amezua balaa kati ya watani wa jadi baada ya Simba kudai kuwa wamezungukwa kwa sababu Mbuyi alishakubali kuwachezea huku wakilishutumu shirikisho la soka nchini na baadhi ya viongozi.
Image
TANZANIA NA UTUMBO WETU . Mashindano ya Olimpiki yamefungwa jana huku washiriki wetu wakirudi mikono mitupu. Katika mchezo wa riadha, Tanzania iliwakilishwa na wakimbiaji wanne ambao ni Zakia Mrisho, Samson Ramadhan, Msenduki Mohamed na Faustine Mussa, waogeleaji wawili ambao ni Ammaar Ghadiyali na Magdalena Moshi na bondia mmoja ambaye ni Selemani Kidunda. Unadhani nini kimesababisha matokeo haya mabaya kabisa Laiti kama mimi ni rais wa Tanzania hawa wote ningewachapa fimbo hazalani na kifungo cha kila mtu miaka miwili miwili naomba mnisamehe mtanzamo tuuu ila tutayafumbia macho mbaka lini .watu wanaojuwa wanachwa na wanapelekwa wasio juwa mwisho wa siku tunavuna utumbo.viongozi achieni ngazi wachukuwe wengine nyie hamna jipya wewe Fibert bayi na wenzako achieni madara kwa wanaojuwa na wenye uchungu na nchi yao. utumbo mtupu huo.kenya na uganda fundisho kwetu hongereni sana kenya na uganda.na poleni Tanzania kwa utumbo wenu.Bayi achia madaraka hayo unakula hela za watu b...