Non chalant na 5o'clock.
Posts
Showing posts from August 27, 2012
- Get link
- X
- Other Apps
Kapombe arejea dimbani MCHEZAJI mahiri wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba, Shomari Kapombe ameanza mazoezi mepesi juzi, baada ya kupona goti lililokuwa likimsumbua kwa siku kadhaa. Kwa mujibu wa daktari wa Simba, Cosmas Kapinga, mchezaji huyo alikuwa anasumbuliwa na goti na kuwa nje ya dimba kwa siku kadhaa. “Tunamshukuru Mungu, Kapombe amepona na kuanza mazoezi, kwa hiyo hatuna majeruhi mwingine, maana (Alex) Sunzu alishapona siku nyingi na leo (jana), amecheza mchezo wa kirafiki na Mathare,” alisema Kapinga. Katika hatua nyingine, Ofisa Habari wa Wekundu hao wa Msimbazi, Ezekiel Kamwaga ‘Mr Liverpool’ alisema, kwa sasa kikosi chao kipo imara na kinaendelea kujifua jijini Arusha ili kuwakabili Azam FC katika mchezo wa Ngao ya Hisani, Septemba 8 pamoja na michezo ya Ligi Kuu. “Kikosi cha Simba kiko vizuri sana kwa sasa, hivyo basi cha kusubiri ni kuonana uwanjani katika mchezo wa Ngao ya Hisani...
- Get link
- X
- Other Apps
Nyota NBA wavutiwa na vipaji Dar WACHEZAJI wa Ligi Kuu ya mpira wa kikapu Marekani (NBA), Hasheem Thabeet na Luol Deng, wamemaliza kliniki ya siku mbili ya mchezo huo kwa vijana jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, huku wakibainisha Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika zenye vijana wenye vipaji. Kliniki hiyo yenye lengo la kusaka vipaji, ilifanyika kwenye kituo cha vijana cha Don Bosco, Upanga na kushirikisha zaidi ya vijana 200, kutoka shule za sekondari mkoani Dar es Salaam. Hii ilikuwa ni kambi ya mafunzo ya pili mwaka huu, chini ya udhamini wa kinywaji cha Sprite, baada ya ile ya awali kufanyika Juni chini ya usimamizi wa Thabeet na kushirikisha vijana chini ya miaka 17 kutoka mikoa mbalimbali nchini. Akichezea timu ya Oklahoma City Thunder ya Marekani, Thabeet ambaye ni kijana wa kwanza wa Kitanzania kucheza ligi maarufu duniani ya NBA, ameahidi kuwa, ataendelea kuunga mkono juhudi za kusaidia mpira wa kikapu nchini, kwa kuendesha klin...
- Get link
- X
- Other Apps
Mazungumzo Tanzania, Malawi yakwama WAKATI mazungumzo ya mgogoro wa mpaka katika Ziwa Nyasa baina ya Serikali za Tanzania na Malawi yakishindwa kupata suluhu, Malawi imetakiwa kusitisha shughuli za utafiti kipindi hiki cha kutafuta muafaka. Hayo yamebainishwa katika mkutano wa wataalamu na viongozi kutoka serikali za nchi hizo baada ya kushindwa kufikia muafaka uliokusudiwa kuhusu eneo halali la mpaka unaozitenganisha. Akizungumza wakati wa kuhitimisha kikao cha usuluhishi kilichohusisha timu za wataalamu na viongozi wa wizara husika wa nchi hizo kilichomalizika juzi usiku mjini Lilongwe, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Bernard Membe, alisema Tanzania bado ina amini katika mazungumzo ili kufikia muafaka. Alisema kuwa pamoja na sababu mbalimbali zilizotolewa na Malawi juu ya umiliki wa eneo lote la Ziwa Nyasa, msimamo wa Tanzania uko wazi kwa kuzingatia vielelezo v...
- Get link
- X
- Other Apps
Mnyukano CCM balaa HARAKATI za baadhi ya vigogo na wapambe wao kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na jumuiya zake, zimeanza kukitisha chama hicho. Tanzania Daima limedokezwa kuwa Kamati Kuu (CC) ya chama hicho iliyokutana Ijumaa iliyopita chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete, imekubaliana kuyafyeka majina yote ya wagombea watakaobainika kushiriki kwenye vitendo vya rushwa na wenye dosari mbalimbali. Akizungumza juzi jijini Dar es Salaam, Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye Nape alisema kuwa CC ilipokea taarifa ya maendeleo ya uchaguzi ndani ya chama na kuridhishwa na uchaguzi huo na kuagiza kila kikao husika kihakikishe haki inatendeka hasa katika uchujaji wa majina ya wagombea. “CC imeagiza kuendelea kukemea vitendo vya rushwa kwenye chaguzi zetu. Na kuhakikisha kila anayebainika kujihusisha na vitendo hivyo au mawakala wao hatua kali za kisheria zitachukuliwa,”alisema. ...
- Get link
- X
- Other Apps
Sensa dosari tupu. • Baadhi ya Waislamu wagomea, wakamatwa SENSA ya watu na makazi iliyoanza jana nchini kote, imegubikwa na kasoro kadhaa katika maeneo mbalimbali, huku suala la uhaba wa vifaa kwa makarani likionekana kuwa kubwa. Tanzania Daima ilifanikiwa kupita kwenye mitaa kadhaa ya mikoa mbalimbali na kuzungumza na wananchi, makarani wa sensa na viongozi wa serikali na kubaini dosari hizo. Hata hivyo, mbali ya uhaba wa vifaa kwa makarani, pia tishio la baadhi ya viongozi wa Kiislamu kuwashawishi waumini wao kususia, nalo lilileta mkanganyiko kwa baadhi ya maeneo. Katika maeneo kadhaa, vilionekana vipeperushi kwenye baadhi ya nyumba vyenye ujumbe wa kuwakataza Waislamu wasishiriki shughuli hiyo, jambo lililowalazimu polisi kusambaa mitaani na kuwatia mbaroni baadhi ya watu waliodaiwa kuvisambaza. Pia, uelewa mdogo wa baadhi ya makarani nao ulilalamikiwa na wananchi wengi, kwani walitumia muda mrefu kuandikisha taarifa zao na hu...
- Get link
- X
- Other Apps
Sensa yaanza Tanzania Tanzania leo imeanza shughuli ya kuhesabu idadi ya watu nchini - shughuli inayofanywa kila baada ya miaka 10. Shughuli zinaendelea ingawa baadhi ya Waislamu wanasema kuwa sensa hiyo imetungwa kwa namna ambayo haitaonesha idadi yao. Waislamu wengine wanasisitiza msimamo wa kutoshiriki iwapo hawataulizwa dini yao. Jumamosi Rais Kikwete aliwasihi watu kwamba ni vema kushiriki kwa ajili ya maendeleo ya nchi
- Get link
- X
- Other Apps
Waziri wa usalama wa Libya ajiuzulu Ripoti kutoka Libya zinaeleza kuwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Fawzi Abdel A'al, amejiuzulu. Hakujatolewa sababu. Inatokea siku moja baada ya polisi katika mji mkuu, Tripoli, kutuhumiwa kuwa hawakufanya kitu kuwazuwia Waislamu wa msimamo mkali wasibomowe msikiti na kaburi la Wasufi mchana.