WABUNGE WAONGEZEWA MARUPU RUPU MJENGONI. MARUPURUPU ya wabunge ikiwamo mishahara imeongezwa kutoka Sh7.4 milioni kwa mwezi hadi takriban Sh11milioni kwa mwezi, hatua ambayo imeibua mjadala mwingine mzito miongoni mwao. Tangu mwaka jana, wabunge wamekuwa katika vita ya kupokea au kutopokea posho ya vikao ambayo imekuwa ikikolezwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe ambaye alizikataa akisema mbunge anapokuwa kazini hahitaji kulipwa. Hata hivyo, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba sasa vita kubwa ipo katika marupurupu mapya ambayo pamoja na kuchanganya na mshahara yanafikia Sh11milioni kwa mwezi. Spika wa Bunge, Anne Makinda alipoulizwa jana alithibitisha kuhusu kuongezeka kwa malipo jumla ya wabunge kwa mwezi lakini akasema hafahamu kiwango halisi kilichoongezwa. Makinda alisema nyongeza iliyopo siyo kwa wabunge tu, bali watumishi wote wa Serikali na ilitangazwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (M...