Posts

Showing posts from April 4, 2014
Image
MASOGANGE  DAH!!!!!!!!!!!!EMBU MUANGALIA SUPERSTAR WETU WA BONGO .
Ngorongoro Heroes waahidi ushindi 04/04/2014 | Posted by  Akidajr | Michezo | 0 comments | 55 views NAHODHA wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’, Aishi Manula, amesema wamejipanga kwa ajili ya kupata ushindi kwenye mechi dhidi ya Kenya itakayochezwa mji wa Machakos, Jumapili. Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhiwa bendera timu hiyo katika ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), jana, Manula ambaye pia anaidakia Azam FC, alisema lengo lao ni kufanya vizuri kwenye mechi hiyo. Naibu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juliana Yasoda, akikabidhi bendera ya taifa, aliwataka wachezaji hao kujituma na kutanguliza uzalendo mbele bila kusahau kuwa mchezo wa mpira wa miguu ni ushirikiano. Alisema Tanzania ina wachezaji wengi wenye vipaji, hivyo waliop...
Image
  SAMATA....SAMATA...SAMATA KILA KONA  YA CONGO AIRUDISHA  TP MAZEMBE NANE BORA  KLABU BINGWA       KLABU ya TP Mazembe imefuzu kutinga Hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Sewe Sport ya Ivory Coast 1-0 jioni hii Uwanja wa Kamalondo mjini Lubumbashi. Mazembe imesonga mbele kwa faida ya bao la ugenini baada ya sare ya jumla ya 2-2 kufuatia awali kufungwa 2-1 mjini Abidjan Jumapili iliyopita. Alikuwa ni mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta aliyefunga bao hilo pekee dakika za mwishoni kipindi cha pili na kuirudisha timu hiyo ya DRC kwenye hatua ya makundi tangu mwaka 2012 waliposhiriki mara ya mwisho. Samatta pia ndiye aliyefunga bao la Mazembe Abidjan ikifungwa 2-1 na maana yake yeye ndiye ameibeba kwa mabega yake timu hiyo hadi Nane Bora na sasa itasubiri kujua wapinzani wake watatu katika droo itakayopangwa Aprili 29 mjini Cairo.
Image
WEMA  AMWAGA CHECHE  KWENYE  OFISI ZA    GLOBAL HOVYOOO! Wema Isaac Sepetu aliye pia Miss Tanzania 2006, amejitoa fahamu kwa kupandisha mzuka na kutinga makao makuu ya Kampuni ya Global Publishers, Bamaga-Mwenge, Dar na kuzua timbwili la aina yake kisa kikiwa ni kuandikwa kwa habari zake na mpenziwe, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’. Tukio hilo la kumchoresha staa huyo mwenye vituko kila kukicha, lilijiri Jumatatu iliyopita kwenye ofisi za Global ambao ni wachapishaji wa gazeti hili (Amani), Uwazi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Championi na Risasi majira ya mchana kweupe hivyo kufunga mtaa huku wapita njia wakimzodoa kwa maneno ya kejeli. Wema akiwa ndani ya ofisi za Global na sura ya ‘kuua mtu’, mkononi akiwa na gazeti la Ijumaa Wikienda lenye stori: DIAMOND ATAMANI USHOGA. Kushoto ni mpambe na mfanyakazi wake Petit Man Wakuache. ATINGA NA WAPAMBE DHAIFU Akiwa na kundi la wapambe dhaifu na goigoi wakiongozwa na meneja wake, M...