Posts

Showing posts from September 26, 2012
Image
BODABODA YASABABIASHA AJALI MOROGORO Mashuhuda waliofika eneo la ajali wakati polisi wa usalama barabarani akishughulikia tatizo hilo. Chanzo cha ajali kikiendelea kuchunguzwa, na mashuhuda wakiendelea kushangaa. Mwenye pikipiki akichukua 'mashine' yake iliyohusika katika ajali. LICHA ya jitihada za jeshi la polisi mkoani  Morogoro kuwaelimisha madereva  wa bodaboda (waendesha pikipiki za biashara), bado wameendelea kusababisha ajali zinazoweza kuepukika. Leo jioni dereva wa bodaboda yenye namba za usajili T 26O BYN aina ya Sanlg aligongwa kwa nyuma na gari aina ya Hiace baada ya kusimama ghafla wakati akiendesha kwa kasi kupita eneo ambalo aliamriwa na askari wa usalama barabarani asimame. Hakuna aliyeumia katika ajali hiyo.