LIGI KUU TANZANIA BARA YA UNGURUMA LEO KWENYE VIWANYA MBALI MBALI :HUKU JANGWANI WAKIANGUKIA PUA NA MNYAMA AKIENDELEZA UBABE WAKE. Watoto wa Jangwani Dar es Salaam Young africans wameendeleza mwanzo mbaya wa Ligi Kuu Tanzania bara baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-0 toka kwa wakata miwa Mtibwa Sugar. Wakati huo Mnyama ameendelea kuunguruma uwanja wa Taifa baada kuichapa JKT Ruvu 2-0 Kwa mabao ya Amri Kiemba na Haruna Moshi Boban, pamoja na kucheza pungufu baada ya Emmanuel Okwi kupewa kadi nyekundu kipindi cha kwanza. Matokeo zaidi soma ubao wa matokeo wa Kili.
Posts
Showing posts from September 19, 2012
- Get link
- X
- Other Apps
BASATA WAMJIA JUU AUNT EZEKIEL Stori:Moodyie SAGA la mwigizaji wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel (pichani) kuvaa nusu utupu na kukaa kihasara huku maungo nyeti yakichungulia, limechukua sura mpya baada ya Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kumjia juu, Ijumaa Wikienda linafunguka. Kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa Basata, Ghonche Materego, wasanii wamekuwa wakionywa mara kwa mara kuhusu kuzingatia maadili na kuacha kuvaa nguo za nusu uchi hivyo inapotokea mmoja wao akawa kichwa ngumu, basi huyo atakuwa na ugonjwa akilini hivyo anahitaji ushauri wa kisaikolojia. “Huyo Aunt Ezekiel anahitaji ushauri nasaha kama ambavyo tumekuwa tukifanya kwa watu wengine wenye tatizo kama lake. Anapaswa kusikiliza maelekezo ya Basata kwamba nguo zisizo na maadili ya Mtanzania hazitakiwi katika sanaa yetu, aache mara moja. “Kila Jumatatu huwa tuna Jukwaa la Sanaa hivyo tumeshakutana na wasanii hao na kuwaeleza tatizo hilo lakini wamekuwa wagumu wa kue...
- Get link
- X
- Other Apps
BREAKING NEWS: WAFUASI WA CHADEMA WAANDAMANA KWA AMANI MKOANI MORO chanzo cha habari global publisher. Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa, John Heche akiongea na wafuasi wa Chadema kwenye ofisi za chama hicho eneo la Kingo. Maandamano yakiongozwa na askari waliokuwa wakidumisha ulinzi. Maandamano ya Chadema yakiendelea mkoani Moro. Wafuasi wa Chadema wakiandamana jioni hii. Mama huyu nae aliamua kuwaunga mkono Wanachadema. WAFUASI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani Morogoro, jioni hii wameandamana kwa amani kutoka maeneo ya Nane Nane walipokwenda kumpokea Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa, John Heche hadi ofisi za makao makuu ya chama hicho ya mkoani hapa, yaliyopo mtaa wa Kingo. Baada ya kufika kwenye ofisi hizo, Heche alizungumza na wafuasi wa chama hicho.