Posts

Showing posts from July 26, 2012
Image
MKWERE AFICHUA UTAMU WA NDOA . MCHEKESHAJI wa Kundi la Kashikashi linalorusha michezo yake kupitia Kipindi cha Mizengwe cha ITV, Hemed Maliyaga ‘Mkwere’ ameweka wazi utamu anaouona kwenye ndoa hivi sasa. Akichonga na Motomoto Newz, Mkwere ambaye alifunga ndoa mwaka jana na Fatma Abadallah na wamepata mtoto mmoja, alisema anaifurahia ndoa yake kiasi kwamba anajilaumu ni kwa nini hakufanya hivyo mapema. “Yaani ndoa ni tamu jamani, nafurahia mazuri mengi ninayofanyiwa na mke wangu, hata uzito wa mwili wangu umeongezeka, nawaomba wale ‘mabachela’ waoe sasa ili waone raha iliyomo ndani ya ndoa,” alisema Mkwere.
Image
  USHUHUDA. WAUMINI wa dini mbalimbali Jumapili iliyopita walijitokeza mbele ya Kanisa la Maombezi lililopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam kumshukuru na kutoa ushuhuda wao wa kupona Ukimwi. Hali hiyo ambayo ilizua msisimko mkubwa kanisani hapo, ilishuhudiwa na mwandishi wetu ambapo watu zaidi ya kumi walionesha vyeti vyao baada ya kupimwa katika hospitali tofauti na kuthibitishwa kupona maradhi hayo. Umati uliokuwepo kanisani hapo ulikuwa ukipiga vigelegele kuthibitisha kuwa walikuwa wamepona... ...baada ya kupata maombezi ya Nabii Flora. Mwandishi wetu alipata nafasi ya kufanya mahojiano na baadhi ya waumini wa kanisa hilo ambao wengi wao waliyasifu maombezi ya Nabii Flora na kusema kuwa ni mazito na yenye kuponya magonjwa sugu. “Pia yanasaidia kurudisha ndugu waliopotea na kuwarejesha pamoja watu walioachana kwa muda mrefu,” alisema muumini mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Merry Lwaluu. BAADHI YA WALIOTOA USHUHUDA Mwandishi wetu alifanikiwa kuwahoji baadh...
Image
Soka ya wanawake yafungua Olimpiki. Mashindano ya kwanza yameanza katika Olimpiki ya mwaka huu, licha ya kwamba michezo hii inafunguliwa rasmi hapo Ijumaa. Akina dada wa timu ya soka, Uingereza wanachuana na New Zealand katika mechi ya soka ya wanawake , mji mkuu wa Wales, Cardiff. Mwandishi wa BBC amesema licha ya iketi chache za mechi hio kununuliwa, mechi ya leo imevutia mashabiki wengi. Mapema leo serikali ya Uingereza ilipongeza hatua ya vyama vya wafanyikazi kufuta mgomo uliopangwa mkesha wa ufunguzi wa Olimpiki na wafanyikazi wa idara ya uhamiaji. Mgomo huu ulitishia kuvuruga shughuli katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Heathrow..  
Image
AZAM na VITAL  VITANI. Vilabu vya Azam na Vita vimefanikiwa kuingia nusu fainali ya michuano ya soka ya Cecafa. John Bocco alikuwa shujaa pale timu yake ya Azam ya Tanzania, ilipofanikiwa kuingia nusu fainali ya mashindano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati baada ya kuwafunga mabingwa wa Tanzania, Simba, mabao 3-1. Katika mechi hiyo ya robo fainali iliyochezwa Jumanne mjini Dar es Salaam, Bocco alifunga mabao yote dakika ya 17, 46 na 73, wakati bao la kufutia machozi la Simba lilifungwa na Shomari Kapombe dakika ya 53. Timu hiyo sasa itapambana na Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kwenye nusu fainali itakayochezwa Alhamisi. Vita Club walifuzu baada ya kushinda kwa mambao 2-1 dhidi ya Atletico ya Burundi kwenye mechi nyingine iliyochezwa Jumanne. Mabao ya Vita yalifungwa na Taddy Etekiama na Basilua Makola wakati bao la Atletico lilifungwa na Pierre Kwizera. Ma...