Taarifa kwa Vyombo vya Habari Vodacom Kutoa Tuzo Kwa waandishi mahiri kumi wa mitandao ya jamii na tovuti Nchini. · Waandishi wa mitandao ya kijamii na tovuti kupewa tuzo kutokana na jitihada na mafanikio yao. · Tuzo hizo kuitwa “ Tuzo za umahiri wa digitali za Vodacom” Dar es Salaam, 11 julai, 2012 Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, itatoa tuzo kwa waandishi bora kumi mahiri katika mitandao ya kijamii kutokana na umahiri wao. Tuzo hizo ambazo zimepewa jina la “Tuzo za Umahiri wa Digitali za Vodacom”, zitatolewa kwa washindi kumi kutokana na jitihada zao na mafanikio yao ikiwa ni kwa mala ya Kwanza kufanywa na kampuni ya simu za Mkononi ya Vodacom. Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Rene Meza amesema kuwa Waandishi wa mitandao ya kijamii wanao mchango mkubwa katika kutoa taarifa mbalimbali ndani ya jamii, na mchango huu unatakiwa kuthaminiwa. Wapo waandishi wengi katika mitandao ya kijamii na wanaandika masuala mbalimbali kuhusu...
Posts
Showing posts from July 11, 2012