| Kitaeleweka: Liverpool, Man City zatunishiana misuli | ||
ONDON, ENGLAND
LIGI Kuu England imeanza tangu wiki iliyopita, lakini utamu halisi utaanza kesho Jumapili wakati Liverpool na Manchester City zitakapokwaana katika Uwanja wa Anfield. Kila kikosi kitaingia uwanjani kusaka ushindi, Manchester City inataka kuendeleza ubabe baada ya kuinyoa Southampton mabao 3-2 wikiendi iliyopita ikiwa ni ushindi wa tano katika mechi tano za karibuni. Kwa upande wake, Liverpool haiwezi kukubali kuwa wateja kwa mara nyingine kufuatia kufungwa mabao 3-0 na West Brom wiki iliyopita. Manchester City inakwenda katika mechi hiyo ikiwa na historia nzuri katika siku za karibuni, lakini timu hizo zilipokutana katika mechi tano za nyuma, Liverpool ilipata ushindi mara mbili, Manchester City mara moja na walitoka sare katika mechi mbili. Liverpool haitakuwa na beki Daniel Agger, ambaye amefungiwa mechi moja na Manchester City itawakosa wachezaji watatu ambao wameumia. Mshambuliaji, Sergio Aguero, kiungo Gareth Barry na beki Micah Richards wote ni majeruhi. Ukiachilia mbali mechi hiyo, Manchester United ambayo Jumatatu wiki hii ilikaribishwa katika ligi kwa kichapo cha bao 1-0 kutoka Everton, huenda ikazinduka wakati itakapokutana na Fulham leo Jumamosi. Manchester United imenasa nyota wazuri kama Shinji Kagawa na Robin van Persie, lakini ilishindwa kutamba mbele ya Everton. Baada ya mechi hiyo kocha, Alex Ferguson, alikiri kufanya makosa kutomwanzisha Van Persie katika kikosi cha kwanza na badala yake nyota huyo aliingia uwanjani dakika 22 kabla ya kipenga cha mwisho Hata hivyo wapinzani wao Fulham wapo katika hali nzuri baada ya kuisambaratisha Norwich City mabao 5-0 katika mechi ya fungua dimba. Nayo Chelsea itakuwa na wakati mgumu itakapoivaa Newcastle United leo Jumamosi. Katika mechi ya awali Chelsea iliifunga Wigan Athletics mabao 2-0 na katikati ya wiki hii iliinyuka Reading mabao 4-2. Hata hivyo Newcastle United ambayo ilimaliza msimu uliopita katika nafasi ya tano juu ya Chelsea, ilianza ligi kwa kutoa kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Tottenham. Nayo Arsenal ambayo ilianza ligi kwa suluhu dhidi ya Sunderland, itataka kuzinduka wakati itakapokuwa ugenini kupambana na Stoke City kesho Jumapili wakati Tottenham itakwaaana na West Brom leo Jumamosi. |
Je! Mavazi ya Polisi wa Kike yanakidhi matakwa ya Waraka Na 3 wa Mavazi ya Watumishi wa Umma? Baadhi ya wadau wamehoji mavazi ya namna hii kwa Asakri Polisi wa Kike kama yanakidhi matakwa na kuweza kumsitiri Askari wa kike wa Jeshi la Polisi awapo katika Utekelezaji wa Kazi zake za kila siku kwa kuwahudumia wananchi. Pia wadau wanahoji kuwa Waraka wa Utumishi wa Umma na 3 wa mwaka 2007 kuhusu mavazi kwa watumishi wa umma kama unatekelezwa na Jeshi jeshi hilo ama au wahusu. Aidha wadau hao wamesema ipo haja kwa Jeshi la Polisi hapa nchini kubadili mavazi hayo kwa Wanawake na kuamuru zivaliwe surwale wakati wote wawapo kazini maana wapo askari wa kikle wanaoenda doria na sketi hizo jambo ambalo ni rahisi kutokea vitendo vya uzalilishaji kwao, na badala yake wameshauri zivaliwe wakati wa shughuli maalum tu kama vile sherehe za kijeshi na Kitaifa ambapo hakuihitaji pilika pilika za hapa na pale ndio wavae Sketi huku pia wakidai sketi hizo ziwe ndefu kia...

Comments
Post a Comment