Posts

Showing posts from June 6, 2012
Image
Marekani yathibitisha kuua al-Libi Ikulu ya White House imesema kwamba imekabili kundi la kigaidi la Al Qaida pigo kubwa kwa kumwua naibu wa mkuu wa kundi hilo, Abu Yahya al-Libi, nchini Pakistan. Maafisa wa Marekani wamesema kuwa alilengwa katika shambulio lilolofanywa na ndege isiyo na rubani ya Marekani katika maeneo ya mashambani ya Pakistan mnamo Jumatatu. Ikulu ya White Housae ilithibitisha kuwa hii ni mara ya pili chini ya muda wa mwaka mmoja ambapo Marekani imemwua kiongozi mkuu wa Al-Qaida, hatua ambayo inakaribia kuangamiza kundi hilo la kigaidi. Afisa wa cheo cha juu katika serikali ya Marekani, amethibitishia BBC kuwa shambulio la ndege isiyo na rubani lililofanywa ...
Rais wa mpito wa Mali yupo salama. Wakuu wa serikali nchini Mali wamesema kuwa Rais wa Mpito, Dioncounda Traore, amepelekwa eneo salama baada ya kupigwa hadi kuzirai na mamia ya waandamanaji nchini humo. Raia hawataki kipindi cha mpito kiongezwe    Mamia ya waandamanaji walimshambulia Rais Traoure wakipinga mkataba ulioafikiwa na Tume ya kiuchumi ya nchi za magharibi mwa Afrika, ECOWAS, ambapo Traoure ataendelea kutawala kwa hadi mwaka mmoja badala ya siku 40 pekee zilizokubaliwa miezi miwili iliyopita. Mwandishi wa BBC amesema kuwa shambulio hilo litawashtua wanadiplomasia waliokuwa wakifanya kila juhudi kurejesha amani na utangamano nchini humo. Muda wa kuongoza aliopewa kiongozi huyo, Djouncounda Traore ulitarajiwa kukamilika Jumatatu. Lakini viongozi wa nchin za Magharibi mwa Afrika, waliafikia ...