Mamilioni kwa watakaowafich ua al-shabaab. Serikali ya Marekani imetenga dola milioni 33 kwa watakaotoa ta arifa zitakazopelekea kukamatwa kwa viongozi saba wa kundi la al-shabab nchini Somalia. Marekani na wachambuzi wengine wa masuala ya usalama wamehusisha kundi hilo na lile la al Qaeda. Viongozi hao ni pamoja na kiongozi mkuu zaidi Mohamed Abdi aw-Mohamed, maarufu Sheikh Mukhtar Abu Zubeyr au jina lingine Ina Gudane yaani mtoto wa Godane. Ndiye muasisi wa kundi hilo. Marekani itatoa dola milioni saba kwa atakayetoa taarifa za kupelekea kukamatwa kwake. Pia katika orodha hiyo ni waanzilishi wengine, Ibrahim Haji Jama, au Ibrahim Afghani - kwa maana asili yake ni Afghanistan. Fu'ad Mohamed Khalf jina lingine ni Shongole,huyu ni mfadhili wa kundi hilo. Amekuwa mmoja wa viongozi wa kuu katika kundi la zamani la mahakama za kiislamu lililoondolewa na wanajeshi wa Ethiopia mwaka 2006. ...
Posts
Showing posts from June 9, 2012