Posts

Showing posts from April 20, 2014
Image
MAMA KIKWETE AWAASA WALIMU NA WAZAZI KUSIMAMIA WATOTO VYEMA KATIKA ELIMU Na Anna Nkinda- Maelezo, Lindi Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi   (CCM) Taifa (NEC) wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete amewataka wazazi na walimu kushirikiana kwa pamoja na kuhakikisha wanafunzi wanakwenda shule na kusoma   jambo ambalo litasaidia kupanda kwa kiwango cha elimu mkoani humo. Mama Kikwete ambaye pia ni Mke wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete alitoa rai hiyo hivi karibuni wakati akiongea na wananchi pamoja   na wanafunzi wa kijiji cha Ruaha waliofika kumsalimia mara baada ya kumaliza mkutano wake   na viongozi wa Halmashauri kuu ya tawi la Ruaha lililopo   katika kata ya Mingoyo   wilaya ya Lindi mjini. Mjumbe huyo wa Halmashauri Kuu Taifa   alisema kiwango cha elimu katika mkoa huo kiko chini lakini kama wazazi watahakikisha watoto wao wanaenda shule kwa wakati na walimu wakihakikisha watoto wamefika shule na kuwafundisha kiw...
Image
AZAM FC YAKABIDHIWA KOMBE LAO RASMI CHAMAZI, SIMBA IKIENDA SARE NA YANGA TAIFA  Wachezaji wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Azam FC ya Chamazi Dar es Salaam wakishangilia baada ya kuweka historia ya kutwaa Ubingwa wa Soka Tanzania 2013-2014. Ubingwa huo ulikuwa unashikiliwa na Yanga iliyoambulia nafasi ya pili na leo ikitoka sare na Simba 1-1. Mshambuliaji wa timu ya Yanga , Hamis Kiiza (kulia) akiwania mpira na beki wa timu ya Simba, Nassor Masoud, katika mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo.hadi mwisho wa mchezo,matokeni Yanga 1-1 Simba. Mshamuliaji wa pembeni wa timu ya Yanga,Simon Msumva (kulia) akijaribu kuwatoka mabeki wa timu ya Simba, katika mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo.hadi mwisho wa mchezo,matokeni Yanga 1-1 Simba. Mshambuliaji wa timu ya Yanga Didier Kavumbagu (katikati) akiwatoka mabeki wa timu ya Simba katika mchezo wa Ligi ku...
Image
PICHA  NA KIMARA UNITED HAPO KINESI