Posts

Showing posts from June 5, 2012
KUMEIVA HUKO LONDON Chelsea yakamilisha mipango ya Hazard. Klabu ya soka ya England ya Chelsea imetangaza katika tovuti yake kwamba hatimaye imekubaliana na klabu ya Lille ya Ufaransa kwamba mchezaji wa kimataifa ya Ubelgiji, Eden Hazard, atajiunga na klabu hiyo ya Stamford Bridge msimu ujao. Mchezaji huyo, mwenye umri wa miaka 21, tayari afya yake imekaguliwa na klabu ya Chelsea, na imeonekana hana tatizo lolote. Walipochukua ubingwa wa ligi ya klabu bingwa, nilijiuliza, "Kwa nini sio Chelsea?", alisema Hazard. "Kulikuwa na mvutano kati ya Chelsea na Manchester united, lakini binafsi naona Chelsea ndio mradi bora zaidi. Ni klabu cha ajabu." Inaarifiwa kwamba Chelsea wameamua kutoa pauni milioni 32 kumpata kijana huyo, na ambaye akizungumza na kituo cha redio cha nchini Ufaransa, RMC, aliongezea: "Chelsea ni timu changa, na nitakuwa na nafasi bora zaidi ya kucheza." ...