Posts

Showing posts from September 7, 2012
Image
Mashambulizi ya kulipiza kisasi Kenya Ramani ya Kenya Takriban watu kumi na moja wa kabila la Pokomo wameuawa katika mashambulizi mapya ya kulipiza kisasi katika eneo la Tana River,Kusini Mashariki mwa Kenya. Mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo alisema alisikia watu wakipiga mayowe wakati kijiji kimoja kilipokuwa kinashambuliwa na kisha wenyeji kuteketezwa. Eneo hilo ambako zinaishi jamii za kuhamahama ni kitovu cha mizozo ya ardhi na maji kati ya jamii za Orma na Pokomo. Watu wengine kumi walijeruhiwa kwenye uvamizi huo uliotokea usiku wa kuamkia leo. Uvamizi huu umetokea baada ya mashambulizi mengine kutokea mwezi jana ambapo watu 52 kutoka jamii ya Orma wengi wakiwa watoto na wanawake kuuawa kwa kunyongwa na kuteketezwa kiasi cha kutotambulika. Ni katika tukio ambalo lilitajwa kuwa ghasi...