Timu za Tanzania zateswa Uganda
KAMPALA, Uganda
TIMU za Tanzania zimeanza vibaya mashindano ya kikapu ya Kanda ya tano yanayofanyika Kampala, Uganda.
Timu za Tanzania zinazoshiriki mashindano hayo ni ABC, Jeshi Stars, Don Bosco na Savio.
ABC wenyewe walianza kwa kufungwa 73-85 na D-Mark Power, wakati Eagle Wings iliichapa 92-36 Donbosco, huku Jeshi Stars ikichapwa 47-84 na Berco Stars.
Pia katika mechi zilizofuata timu ya Urunani iliichapa Savio 58-51, wakati KCB iliichapa ABC 95-59 na KPA iliishinda Jeshi Stars 91-38.
Juzi timu ya D-Mark Power kutoka Sudan ya Kusini iliichapa ABC 85-73 na kuingia hatua ya nusu fainali.
Wakati huohuo Mwenyekiti wa Baraza la Michezo wa Uganda (NCS), Anthony Katamba amejiuzulu wadhifa wake kwa sababu ya mgogoro wa kuutumia uwanja wa ndani wa Lugogo unaoandaa mashindano hayo ya kikapu ya Kanda ya tano.
Waziri wa Michezo wa Uganda, Charles Bakkabulindi amepokea barua ya Katamba ya kuomba kujiuzulu na amemchagua mjumbe wa Baraza hilo, Bosco Onyik kukaimu nafasi ya mwenyekiti wa NCS.
![]() |

Comments
Post a Comment