Bao la 'offside' la Torres laibeba Chelsea

LONDON, England
MSHAMBULIAJI Fernando Torres alifunga bao la utata na kuisaidia Chelsea kupata ushindi mnono wa mabao 4-2 dhidi ya Reading kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.

Utata wa bao Torres ulikuja baadaye picha ya televisheni ilionyesha mshambuliaji huyo wa Hispania alikuwa ameotea wakati akiunganisha krosi ya Ashley Cole.

Msimu uliopita Torres hakufunga bao lolote hadi mwezi Septemba 18na kufanikiwa kumaliza akiwa amefunga mabao sita tu..

Ni wazi alikuwa ameotea nimeuzunika sana, alisema kocha wa Reading, Brian McDermott, ambaye alipiga bao hilo kwa mwamuzi msaidizi. Ni aibu kubwa kwa mwamuzi kuruhusu bao kama ilo.

Reading waliamka kusaka bao la kusawazisha, lakini Eden Hazard alifanikiwa kuzuia mpira wa adhabu na kuanzisha shambulizi la kushtukiza iliyochangia kupatikana bao la Branislav Ivanovic zikiwa zimebakia dakika tano kabla ya filimbi ya mwisho.

Frank Lampard alifunga bao la kwanza kwa Chelsea dakika ya18 kwa mkwaju wa penalti baada ya Hazard kufanyiwa faulo na Chris Gunter, lakini Reading walifanikiwa kuongoza 2-1 kabla ya mapunziko kwa mabao ya Pavel Pogrebnyak na Danny Guthrie.

Gary Cahill alifunga bao la kusawazisha 2-2 baada ya kipwa wa Reading, Adam Federici kufanya uzembe.

Kocha wa Chelsea, Roberto Di Matteo aliwasifia mshambuliaji wake Hazard aliyemsajili kutoka Lille.

Amekuwa na mchango kubwa kwetu na pia ushirikiano wake na Juan Mata ni mzuri, alisema Di Matteo.

BERNE, Malaga na BATE Borisov wamejiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu kwa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa baada ya kushinda mechi zao kwa ushindi 2-0.

Malaga waliwachapa Panathinaikos 2-0 kwa mabao ya Martin Demichelis na Eliseu.

Wakati Vitali Rodionov alifunga mabao mawili katika dakika ya 29 na 78 kwa mabingwa wa Belarus, BATE walipowachakaza Kiryat Shmona.

Nayo AEL Limassol ilishinda 2-1 nyumbani dhidi ya Anderlecht kwa mabao ya Dossa Junior na Rui Miguel, huku bao la kufutia machozi kwa Anderlecht likifungwa na Deiudonne Mbokani.

Dinamo Zagreb ilichapa Maribor 2-1, wakati Sporting Braga na Udinese zikitoka sare 1-1, mechi za marudiano zitafanyika Jumanne ijayo.

Comments

Popular posts from this blog