SAMATA....SAMATA...SAMATA KILA KONA YA CONGO
AIRUDISHA TP MAZEMBE NANE BORA KLABU BINGWA
KLABU
ya TP Mazembe imefuzu kutinga Hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa
Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Sewe Sport ya Ivory Coast 1-0
jioni hii Uwanja wa Kamalondo mjini Lubumbashi.
Mazembe
imesonga mbele kwa faida ya bao la ugenini baada ya sare ya jumla ya
2-2 kufuatia awali kufungwa 2-1 mjini Abidjan Jumapili iliyopita.


Alikuwa ni mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta aliyefunga bao hilo pekee dakika za mwishoni kipindi cha pili na kuirudisha timu hiyo ya DRC kwenye hatua ya makundi tangu mwaka 2012 waliposhiriki mara ya mwisho. Samatta pia ndiye aliyefunga bao la Mazembe Abidjan ikifungwa 2-1 na maana yake yeye ndiye ameibeba kwa mabega yake timu hiyo hadi Nane Bora na sasa itasubiri kujua wapinzani wake watatu katika droo itakayopangwa Aprili 29 mjini Cairo.
Comments
Post a Comment