Ngorongoro Heroes waahidi ushindi
Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhiwa bendera timu hiyo katika ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), jana, Manula ambaye pia anaidakia Azam FC, alisema lengo lao ni kufanya vizuri kwenye mechi hiyo.
Naibu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juliana Yasoda, akikabidhi bendera ya taifa, aliwataka wachezaji hao kujituma na kutanguliza uzalendo mbele bila kusahau kuwa mchezo wa mpira wa miguu ni ushirikiano.
Alisema Tanzania ina wachezaji wengi wenye vipaji, hivyo waliopata fursa ya kuwemo Ngorongoro Heroes wakati huu, wajue kuwa wamepata bahati na wanatakiwa kufahamu kuwa wao ni wawakilishi wa Tanzania na Watanzania wana kiu ya kusikia matokeo ya mechi hiyo.
Heroes inayofundishwa na John Simkoko, inaondoka leo saa 4:30 asubuhi kwa ndege ya Kenya Airways na mara baada ya kuwasili, itakwenda moja kwa moja kwenye hoteli ya Garden iliyopo Machakos, ambayo ndiyo imepangiwa kufikia na Shirikisho la Soka Kenya (FKF).
Wachezaji waliopo kwenye msafara huo unaoongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Ayoub Nyenzi, ni Abrahman Mohamed, Manula, Ally Idd, Ally Mwale, Athanas Mdamu, Ayoub Semtawa, Bryson Raphael na Edward Manyama.
Wengine ni Gadiel Michael, Hamad Juma, Hassan Mbande, Ibrahim Ahmada, Idd Ally, Kelvin Friday, Michael Mpesa, Mohamed Ibrahim, Mudhathir Yahya, Pato Ngonyani, Peter Manyika na Salum Mineli.
Comments
Post a Comment