VIDEO: Binti wa miaka 5 abakwa na kuuawa na mjomba wake
Wakaazi
wa kijiji cha Kahaini wilayani Maragua wameamkia majonzi baada ya mwili
wa msichana wa miaka mitano kupatikana mita chache kutoka shule
aliyokuwa akihudhuria. Na kama hilo halikuwa kubwa, baya Zaidi,
mjombake mtoto huyo yuko korokoroni baada ya kukiri kumnajisi mpwa wake
kisha akamuua na kuutupa mwili wake. Kuwa unyama umewatoka hayawani na
kuwaingia binadamu, jamaa huyo alidai kuwa pepo ndio waliomtuma
kutekeleza unyama huo.