KALAPINA AONGEA KUHUSU UJIO WA RICK ROSS

Nguli wa Hip hop hapa Bongo, lijulikanalo kama Kikosi cha Mizinga lenye maskani yake pande za Kinondoni jijini Dar, Kalama Masoud Kalapina amesema ujio wa nyota wa muziki huo kutoka Marekani Rick Ross kwenye tamasha la Fiesta 2012 ni zaidi ya shoo kwa wasanii wa Tanzania.
Akizungumza na blog hii mapema leo Kalapina amesema kuwa wasanii wa Bongo hawataakiwi kwenda kwenye shoo ya fiesta kwa ajili ya kupiga picha na mkali huyo kwa ajili ya facebook na twitter ama kwenda kugusa tumbo kwani hazitawasaidia chochote kwenye muziki wao.
Hatutakiwi kwenda kwa ajiri ya facebook na twitter isipokuwa tunatakiwa kwenda kujifunza mbinu anazotumia kutawala jukwaa na pia kujaribu kuzungumza naye kuhusu njia ambazo anatumia kupata mafanikio kimuziki na zaidi kipi kimemfanya kuwa mmoja ya mastaa walioleta mapinduzi kwenye muziki wa sasa alisema Kalapina.
Akiendelea zaidi Kalapina alisema kuwa ujio wa Ross ni kitu kikubwa sana kwenye muziki wetu wa Tanzania na kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuitangaza nchi yetu hivyo anatoa pongezi zote kwa kampuni ya Clouds Media kwa kufanikisha ujio huu.
Comments
Post a Comment