MBUNGE WA VITI MAALUMU IRINGA RITHA KABATI AMJIBU MSIGWA
Mbunge wa viti maalumu Iringa kupitia CCM Ritha Kabati leo
ameongea na wanahabari Iringa kwa kile anachodai kudhalilishwa na mbunge wa
Iringa mjini kupitia tiketi ya CHADEMA Peter Msigwa.
Kabati ameeleza kuwa mbunge huyo amekuwa siku ta tarehe 19
septemba katika mkutano wake uliofanyika katika eneo la soko kuu na kumtaka
aelewe kuwa yeye ni mbunge wa kuteuliwa ambae pia ni mbunge halali ambaye
anaweza kufanya kazi kwa uhuru na kwamba nayonafasi kubwa katika halmashauri ya
mkoa na kueleza
“Nimekuwa nikichukizwa
na tabia ya mbunge huyo kutopenda yeye kutumia nafasi aliyonayo katika kutoa
hoja zainazohusu jimbo la Iringa bungeni kitu ambacho hanitendei haki”. Alisema
Pia amemuomba msigwa kuiga mfano wa wabunge wengine katika
meneo mengine na kuwa na ushirikiano kwa kuacha tofauti zao kwaajili ya
maendeleo ya wananchi wa Iringa na kwa Tanzania kwa ujumla.

Comments
Post a Comment