MASANJA MKANDAMIZAJI AMWAGA MAHUBIRI UBARI.

Emanuel Mgaya
Masanja Mkandamizaji msanii wa vichekesho Mchungaji Mtarajiwa.
MSANII Nyota na mchekeshaji mahiri katika tasnia ya filamu Swahiliwood Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ hivi karibuni alifanya huduma ya mahubiri ya dharura katika mazishi ya mdogo wake aliyejulikana kwa jina la Varerian Mgaya yaliyofanyika huku Mbalali katika Kijiji cha Ubaruku, Masanja alitumia muda aliopewa na familia kwa ajili ya kutoa shukani kwa ndugu na jamaa waliojitokeza katika mazishi hayo yaliyoudhuriwa na mamia ya waombolezaji kutoka sehemu mbalimbali, Masanja alisistiza vijana na jamii nzima kuokoka na kumtumikia Mungu.

Umati wa watu Ubaruku
Umati wa wakazi wa Ubaruku wakimsikiliza Masanja Mkandamizaji haonekani pichani.
Wakazi wa Ubaruku
Wakazi wa Ubaruku wakiwa makini kumsilikilza Mchungaji mtarajiwa Masanja Mkandamizaji.
Alex Chalamila
Mac Reagan akipiga picha katika tukio hilo.
Emanuel Mgaya
Masanja akisikiliza Mhubiri mwenzake katika makaburi ya Ubaruku.
Emanuel Mgaya Mh. Neema Mgaya
Msanja Mkandamizaji akiwa Mh. Neema Mgaya
Emanuel Mgaya
Masanja Mkandamizaji akiwa katika Pozi.
“Binadamu ukifariki hakuna kesi tena ambayo utasema uweke wakili ili akutetee kulinga na dhambi zako, Mbinguni ni hukumu tu kwa mantiki hiyo nawahibiri watu wote waokoke na kumfuata Yesu kwani ndio Mwokozi wetu, mara nyingi ninaposema watu waokoke wanaanza kuniangalia kuanzia chini mpaka juu kisha wanajijubu wenyewe mbona ana marasta hapo ndio unajua kuwa watu hawa hata Biblia hawasomi, ukisoma katika Biblia utagundua kuwa akina Masanja wapo, Samson mnadhiri wa Mungu si alikuwa na Rasta sasa mnashangaa nini hapo?,”anauliza Masanja.
Masanja nasema kuwa vijana wengi wake kwa Waume hawataki kuokoka kwa sababu ya matamanio ambayo ni vitu vya kupita na havina maana yoyote, alisema kuwa yeye anaamini kuwa ni mtu maarufu kupitia Orijino Komedi kipindi ambacho urushwa kupitia Televisheni ya Taifa (TBC1), lakini bado kaona umuhimu wa kuokoka na kumtumikia Mungu haoni sababu ya watu kupoteza muda wote kwa kutomfuata Yesu wakati hata jamii haiwatambui na hayo wanayohangaikia.
Umati wa waombolezaji walifurahia mahubiri hayo ambayo yalikuwa yakiambatana na vichekesho katika mazishi hayo Masanja alifanya mahubiri makaburini baada ya mazishi ambayo pia yaliudhuriwa na Mh. Neema Mgaya Mbunge wa viti maalumu Vijana Taifa, Mac Reagan na wadau wa filamu kutoka sehemu mbalimbili ikiwa na viongozi wa kisiasa na Serikali.

Comments

Popular posts from this blog