BODABODA YASABABIASHA AJALI MOROGORO
LICHA
ya jitihada za jeshi la polisi mkoani Morogoro kuwaelimisha madereva
wa bodaboda (waendesha pikipiki za biashara), bado wameendelea
kusababisha ajali zinazoweza kuepukika.
Leo
jioni dereva wa bodaboda yenye namba za usajili T 26O BYN aina ya Sanlg
aligongwa kwa nyuma na gari aina ya Hiace baada ya kusimama ghafla
wakati akiendesha kwa kasi kupita eneo ambalo aliamriwa na askari wa
usalama barabarani asimame.
Hakuna aliyeumia katika ajali hiyo.
Comments
Post a Comment