Waziri wa usalama wa Libya ajiuzulu
Ripoti kutoka Libya zinaeleza kuwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Fawzi Abdel A'al, amejiuzulu.

Inatokea siku moja baada ya polisi katika mji mkuu, Tripoli, kutuhumiwa kuwa hawakufanya kitu kuwazuwia Waislamu wa msimamo mkali wasibomowe msikiti na kaburi la Wasufi mchana.
Comments
Post a Comment