WABUNGE WAONGEZEWA MARUPU RUPU MJENGONI.
MARUPURUPU
ya wabunge ikiwamo mishahara imeongezwa kutoka Sh7.4 milioni kwa
mwezi hadi takriban Sh11milioni kwa mwezi, hatua ambayo imeibua
mjadala mwingine mzito miongoni mwao.
Tangu
mwaka jana, wabunge wamekuwa katika vita ya kupokea au kutopokea
posho ya vikao ambayo imekuwa ikikolezwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini
(Chadema), Zitto Kabwe ambaye alizikataa akisema mbunge anapokuwa
kazini hahitaji kulipwa.
Hata
hivyo, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba sasa vita kubwa ipo
katika marupurupu mapya ambayo pamoja na kuchanganya na mshahara
yanafikia Sh11milioni kwa mwezi.
Spika
wa Bunge, Anne Makinda alipoulizwa jana alithibitisha kuhusu
kuongezeka kwa malipo jumla ya wabunge kwa mwezi lakini akasema
hafahamu kiwango halisi kilichoongezwa.
Makinda
alisema nyongeza iliyopo siyo kwa wabunge tu, bali watumishi wote wa
Serikali na ilitangazwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Menejimenti
ya Utumishi wa Umma), wakati wa Bajeti ya Ofisi hiyo kwa mwaka
2012/13.
“Hiyo
nyongeza siyo tu kwa wabunge, bali ni kwa watumishi wa Serikali. Tena
hiyo ilitangazwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Menejimenti ya
Utumishi wa Umma). Sasa ukiniuliza kiasi gani hapo ndipo sielewei, ila
najua nyongeza ipo,” alisema Spika.
Lakini,
vyanzo kutoka ndani ya Bunge vilisema kwamba nyongeza hiyo ambayo
tayari imeingia katika mshahara wa Julai ni Sh3.6milioni, hivyo kufanya
jumla ya fedha anazochukua mbunge kufikia kiasi hicho cha Sh11milioni.
“Hiyo ni vita, kuna wabunge wana hasira kweli hawataki wananchi wajue kama marupurupu yameongezeka.
Wanaona
wananchi wakijua itakuwa ni tatizo kubwa, watapigiwa kelele lakini
nyongeza hiyo ipo. Tayari wengine wamechukua tangu Ijumaa,” kilisema
chanzo kimoja kwa sharti la kutotajwa jina gazetini.
Hata
hivyo, kwa mujibu wa chanzo hicho, baadhi ya wabunge kutoka kundi la
wanaopinga posho kwa wabunge wamepinga pia nyongeza hiyo wakitaka
fedha hizo zielekezwe katika sekta nyingine za kijamii.
Marupuru ya sasa
Hadi
mwezi uliopita, mbunge alikuwa akipokea Sh7.4milioni kwa mwezi ambazo
kati ya hizo Sh2.5milioni ni kwa ajili ya mafuta, Sh2.3 mshahara,
Sh170,000 kwa ajili ya mshahara wa dereva, 100,000 kwa ajili ya katibu
wa mbunge na posho ya jimbo.
Hata
hivyo, katika nyongeza hiyo ya sasa haijawekwa wazi kwamba kiasi gani
ni kwa ajili ya mshahara, fedha za mafuta ya gari la mbunge, za
dereva, katibu na za posho ya jimbo na tayari baadhi ya wabunge
wameanza kufuatilia mchanganuo wa nyongeza hiyo.
Chanzo:

Comments
Post a Comment