Vodacom yatengeneza ajira zaidi kwa Watanzania.
KAMPUNI ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, imetangaza kujivunia
wingi wa ajira ambazo imetengeneza kwa Watanzania tangu kuanzishwa
kwake.
Kampuni hiyo imeajiri asilimia kubwa ya Watanzania katika ajira za moja kwa moja na zile zisizo za moja kwa moja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Rene Meza, alitaja maeneo mbalimbali ambayo kampuni hiyo imetoa ajira kwa wingi kuwa ni huduma ya M–pesa ambayo imetengeneza ajira zaidi ya 25,000 kwa watu wa makundi mbalimbali.
“Kama kampuni tuna ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja, kupitia huduma yetu ya M-pesa, sasa tumetengeneza ajira zaidi ya 25,000 hapa nchini; mijini na vijijini.
“Hii ni hatua kubwa sana katika sekta ya ajira. Kwa kuwa huduma hii imeshika hatamu katika huduma za kifedha bado watu wengi zaidi wanaendelea kujiunga na uwakala. Kwa mwezi sasa tunapata maombi ya uwakala zaidi ya 2,000 hivyo tunatarajia ajira hizi kuongezeka kwa kasi,” alisema.
Mkurugenzi huyo alibainisha sehemu nyingine ambazo kampuni hiyo imetoa ajira kwa Watanzania zaidi kwamba kumekuwa na wafanyabiashara wa kujitegemea wapatao 6,000 ambao wamejiajiri kwa kuuza muda wa maongezi na kadi za simu.
“Tumegundua kuwa Watanzania wengi wanaweza kujiajiri na kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo. Tunaona kwa kiasi kikubwa watu waliojiajiri kuwa mawakala wanaendelea vizuri, hivyo tumetengeneza mfumo ambao utaendelea kutoa ajira zaidi za kujitegemea kwa Watanzania na mpango wa kutoa elimu ya biashara kwa watu hawa,” alisema.
Meza aliongeza kuwa kampuni hiyo sasa imetoa ajira za moja kwa moja zaidi ya 450 na kutoa kipaumbele kwa wanawake ambao wanaongoza vitengo mbalimbali vya kampuni hiyo.

Comments
Post a Comment