Skip to main content

Uchaguzi Igunga na Pepo za Mabadiliko Tanzania

Kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu Tanzania wa Oktoba 2010, tumeshuhudia pepo kubwa sana zikivuma kwa kasi kutoka pande zote za nchi yetu. Ni pepo za mabadiliko. Wananchi wanataka madadiliko ya kweli. Watawala walioko kwenye ngazi kubwa za nchi hii ama wamezisikia au kuziona hizo pepo lakini bado hawajaonesha jitihada za kuzizuia. Ni mwanzo wa miti mikubwa yenye nguvu kubwa (Key Politicians) kuangushwa chini na pepo hizo. Ni wakati ambapo watawala hawataamini kilichofanyika.

Mabadiliko haya yamenikumbusha Hotuba makini na ya kihistoria ya Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Mr Hrold Macmillan alipotembelea Afrika na tarehe 3 Februari 1960 na akahutubia maelfu ya watu huko Afrika ya Kusini, na kusema:

"The wind of change is blowing through this continent (Africa), and whether we like it or not, this growth of national consciousness is a political fact. We must all accept it as a fact, and our national policies must take account of it." - Harold Macmillan.

Kwa uchaguzi huu, tutarajie mabadiliko makubwa yanakuja.... Nguvu ya umma ni kila kitu. Wazambia wamefanya. Ni zamu yetu mwaka 2015 kwa kutumia mtaji tulioupata Igunga na kwingineko. Mnasemaje wadau???

Comments

Popular posts from this blog