Tanzania imejaaliwa kuwa na aina nyingi sana za wanyama katika mbuga zetu. Na wao kama viumbe hai kuna wakati wanapata magonjwa yanayotishia uhai wao. Ungekuwa wewe ni daktari wa wanyama ungepata ujasiri wa kutibu wanyama wakali kama Simba, Chui, Mamba au Nyoka
Je! Mavazi ya Polisi wa Kike yanakidhi matakwa ya Waraka Na 3 wa Mavazi ya Watumishi wa Umma? Baadhi ya wadau wamehoji mavazi ya namna hii kwa Asakri Polisi wa Kike kama yanakidhi matakwa na kuweza kumsitiri Askari wa kike wa Jeshi la Polisi awapo katika Utekelezaji wa Kazi zake za kila siku kwa kuwahudumia wananchi. Pia wadau wanahoji kuwa Waraka wa Utumishi wa Umma na 3 wa mwaka 2007 kuhusu mavazi kwa watumishi wa umma kama unatekelezwa na Jeshi jeshi hilo ama au wahusu. Aidha wadau hao wamesema ipo haja kwa Jeshi la Polisi hapa nchini kubadili mavazi hayo kwa Wanawake na kuamuru zivaliwe surwale wakati wote wawapo kazini maana wapo askari wa kikle wanaoenda doria na sketi hizo jambo ambalo ni rahisi kutokea vitendo vya uzalilishaji kwao, na badala yake wameshauri zivaliwe wakati wa shughuli maalum tu kama vile sherehe za kijeshi na Kitaifa ambapo hakuihitaji pilika pilika za hapa na pale ndio wavae Sketi huku pia wakidai sketi hizo ziwe ndefu kia...

Comments
Post a Comment