Mrwanda kutimkia Ufaransa.
BAADA ya kufunga ndoa Danny Mrwanda ameweka bayana kuwa anadhamiria kutimkia Ufaransa, Mwanaspoti lina taarifa kamili.
Nyota huyo ana malengo ya kwenda huko na ikishindikana atarudi Vietnam alikokuwa akicheza soka lake awali.
"Natarajia kuondoka kwenda Ufaransa kwa mujibu wa wakala wangu, lakini ikishindikana nitarudi Vietnam nilikokuwa nacheza awali.
"Nitaondoka baada ya kufunga ndoa Septemba 7 lakini nasubiri barua ya kuachwa kutoka Simba,"alisema.
Akizungumzia kuachwa kwake, Mrwanda alisema ni jambo la kawaida katika maisha ya soka.
Mrwanda hajajumuishwa katika kikosi cha Simba kitakachocheza msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara licha ya kufikia nayo makubaliano na kucheza mechi za Kombe la Urafiki na Kagame ingawa alishindwa kuonyesha kiwango.
Kocha mpya Azam akuna kichwa
KOCHA Mkuu wa Azam FC, Mserbia Boris Bunjak amekiri yupo katika wakati mgumu kipindi hiki kukirudishia makali kikosi cha timu hiyo yenye maskani yake Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Kocha huyo alichukua mikoba baada ya Mwingereza Stewart Hall kufukuzwa kazi.
Bunjak amesema tangu afike hapa nchini na kupewa kazi ya kukinoa kikosi hicho takriban siku 11 zimepita bado hajapata kikosi cha kutamba msimu huu.
Aliongeza kuwa muda wa siku zilizobaki kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara haumtoshi lakini atatumia akili za ziada kupandisha kiwango cha timu.
"Siwezi kusema chochote juu ya maandalizi ya timu yangu katika msimu mpya wa ligi muda nilionao ni mdogo kuandaa timu yangu ya ushindi ukizingatia morali wa timu umeshuka tofauti na nilivyotegemea kwa hiyo lolote linaweza kutokea.
"Ukiangalia mechi zetu mbili tulizocheza na Simba na ile ya Polisi Morogoro siwezi kusema ni kipimo kizuri kwa timu yangu katika maandalizi ya ligi kwa hiyo nina kazi kubwa katika muda huu mfupi uliobaki.
Nahitaji kuitengeneza timu kisaikolojia ukizingatia kuna mwenzangu aliyepita hapa ambaye alikuwa na mifumo yake. Nitajitahidi kuhakikisha tunafanya kweli kulingana na kasi ya timu, "alisisitiza.
Kocha Stars akubali muziki wa Simba .
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amesema mshambuliaji kinda wa Simba, Edward Christopher pamoja na mabeki wa kikosi hicho wanatakiwa kutunzwa kutokana na kazi kubwa na uwezo walioonyesha kwa kupambana na timu za Ligi Kuu Bara kwenye michuano ya BancABC Super 8.
Bosi huyo licha ya kutotoka kusema kama atawapa nafasi kubwa kwenye timu yake lakini alivutiwa na wachezaji wa timu hiyo na kuwaambia wasaidizi wake kwamba wanahitaji kumtathmini kila mchezaji wa timu hiyo kwa jicho la pili.
Alisema kuanzia mchezo wa kwanza mpaka mwisho wachezaji waliokuwa wakibadilishana namba kwenye ukuta walicheza vizuri hata washambuliaji walionyesha juhudi na kwamba Simba inastahili pongezi.
Kocha huyo alisema umefika wakati wa makocha wa timu kubwa kuwapa nafasi yosso katika timu za wakubwa na kuwaamini kuwa wanaweza wasiishie tu kwenye kushiriki mashindano ya msimu hadi msimu kwani kufanya hivyo ni kuwapotezea malengo chipukizi hao.
"Vijana wanaweza hii ni changamoto kwa klabu kubwa na pia makocha na viongozi kuwaamini vijana hawa na kuwapa nafasi isiishie kwenye mashindano tu, hii ni hazina kubwa ya taifa katika kipindi ambacho tupo katika mipango ya kutengeneza Stars bora,"alisisitiza kocha huyo.
Simba B ilitwaa Kombe la Super 8 wikiendi iliyopita baada ya kuifunga Mtibwa Sugar mabao 4-3.
Samatta aonyesha maajabu Misri.
HAKUNA ubishi! Staa wa Tanzania, Mbwana Samatta amedhihirisha kuwa ndiye kiboko cha Wamisri.
Hiyo ni habari njema kwa wadau wa soka kwani, timu za Tanzania zimekuwa zikinyanyasika kwa timu za Misri na tangu kupata uhuru mwaka 1961.
Simba ndiyo timu pekee ya Tanzania kuwahi kuitoa timu ya Misri, pale ilipoing'oa Zamalek mwaka 2003, ambayo pia ilionja joto ya jiwe kwa Samatta, juzi Jumapili.
Samatta alidhihirisha ana nyota ya kuwatungua Wamisri kwenye Uwanja wa Chuo cha Jeshi la Misri uliopo jijini Cairo, wakati alipofunga bao la ushindi dakika ya 42 wakati timu yake ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilipoilaza Zamalek ya Misri mabao 2-1.
Mtanzania huyo alifunga bao hilo baada ya kuunganisha kwa kichwa mpira wa juu uliobetuliwa na Tresor Mputu.
TP Mazembe ndiyo ilitangulia kufunga mapema katika kipindi cha kwanza lakini Zamalek ilisawazisha muda mfupi baadaye.
Hii ni mara ya pili kwa Samatta kuwafunga Zamalek kwani katika mchezo wa kwanza uliochezwa hivi karibuni mjini Lubumbashi alifunga pia wakati TP Mazembe ilipopata ushindi wa 2-0.
Samatta pia alizamisha bao katika uwanja huo wa Jeshi la Misri, TP Mazembe ilipolizwa na Al-Ahly 2-1.

Comments
Post a Comment