Kocha wa Kuwait apigwa risasi

Goran Tufegdzic
Polisi ya Serbia inasema kuwa
kocha wa timu ya Taifa ya Kuwait Goran Tufegdzic ameuawa kwa kupigwa
risasi nchini mwao Serbia na hali yake imesemekana ni mbaya.
Polisi katika mji wa Pozarevac ulio katikati mwa
nchi wamesema kuwa Bw.Tufegdzic alipigwa risasi ya kifua siku ya ijumaa
baada ya ugomvi na jirani juu ya kipande cha ardhi. Baada ya hapo
alimpiga risasi na kukimbizwa hadi hospitali ya mjini Belgrade.Tufegdzic, ambaye amefanya kazi huko Mashariki ya kati kwa takriban miaka kumi aliteuliwa kama kocha wa Kuwait mwaka 2009. Aliiwezesha timu hio kufuzu kushiriki kombe la mataifa ya bara Asia la mwaka 2010 na kuisaidia kushinda kombe la mataifa ya Ghuba la mwaka 2010.
Mwenyekiti wa chama cha mpira cha Kuwait Sheik Talal Al-Sabah anasema kuwa amezungumza na mke wa kocha huyo na ana matumaini atapata nafuu na kwamba familia yake itaweza kupitia kipindi hiki kigumu''
Comments
Post a Comment