Kapombe arejea dimbani


MCHEZAJI mahiri wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba, Shomari Kapombe ameanza mazoezi mepesi juzi, baada ya kupona goti lililokuwa likimsumbua kwa siku kadhaa.
Kwa mujibu wa daktari wa Simba, Cosmas Kapinga, mchezaji huyo alikuwa anasumbuliwa na goti na kuwa nje ya dimba kwa siku kadhaa.
“Tunamshukuru Mungu, Kapombe amepona na kuanza mazoezi, kwa hiyo hatuna majeruhi mwingine, maana (Alex) Sunzu alishapona siku nyingi na leo (jana), amecheza mchezo wa kirafiki na Mathare,” alisema Kapinga.
Katika hatua nyingine, Ofisa Habari wa Wekundu hao wa Msimbazi, Ezekiel Kamwaga ‘Mr Liverpool’ alisema, kwa sasa kikosi chao kipo imara na kinaendelea kujifua jijini Arusha ili kuwakabili Azam FC katika mchezo wa Ngao ya Hisani, Septemba 8 pamoja na michezo ya Ligi Kuu.
“Kikosi cha Simba kiko vizuri sana kwa sasa, hivyo basi cha kusubiri ni kuonana uwanjani katika mchezo wa Ngao ya Hisani na Ligi Kuu, maana kwa sasa tusiandikie mate wakati wino upo,” alisema Kamwaga.
Kikosi cha Simba kipo mjini Arusha takribani wiki tatu sasa kikijinoa.


Comments

Popular posts from this blog