KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Nizar Khalfan, ameondolewa katika kikosi
cha timu hiyo kinachoshiriki Kombe la Kagame kufuatia kushtua nyonga.
Nizar ambaye amesajiliwa na Yanga msimu huu baada ya kutemwa na klabu ya Philadelphia Union ya Marekani, kabla ya kupata majeraha hayo alikuwa tayari ameshatupia nyavuni bao moja katika michuano hiyo.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Daktari wa Yanga, Juma Sufiani, alisema Nizar aliumia Ijumaa iliyopita wakati timu hiyo ikicheza dhidi ya APR ya Rwanda ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kutinga katika hatua ya robo fainali.
Leo, Yanga wataanza changamoto ya kucheza michuano ya Kombe la Kagame bila kiungo huyo katika mchezo wa robo fainali dhidi ya Mafunzo ya Zanzibar, unaotarajiwa kuchezwa kuanzia saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Sufiani alisema kiungo huyo atakuwa nje kwa muda wa wiki mbili, ikiwa na maana kwamba huenda asionekane tena katika michuano hiyo kwa mwaka huu, hata kama Yanga itafanikiwa kufika fainali.
“Mara baada ya kuumia katika mchezo ule dhidi ya APR tulikuwa tunamfanyia mazoezi madogo lakini ameonekana akizidi kulalamika maumivu hali ambayo imetulazimu tumpe muda wa mapumziko ili apone taratibu,” alisema Sufiani.

Comments
Post a Comment