GLOBAL PUBLISHERS YATOA POLE KWA WALIOFIKWA NA AJALI YA MV SKAGIT.

 

KAMPUNI ya Global Publishers & General Enterprises Ltd, imepokea kwa masikitiko taarifa za kuzama kwa Meli ya MV Skagit jana eneo la Chumbe jirani na Bandari ya Zanzibar.
Meli hiyo iliyokuwa na watu wanaokadiriwa kuwa 290 ilizama wakati ikitokea Dar es Salaam kuelekea Unguja, Zanzibar. Maiti zaidi ya 30 mpaka sasa zimeokolewa kutoka baharini na zoezi la uokoaji linaendelea.
Tunaungana na Watanzania wote kutoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki waliofikwa na tukio hili.
Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu wote mahali pema peponi.
INNA LILLAH WA INNA ILLAYH RAJIUUN.

Comments

Popular posts from this blog